Watuhumiwa wa Ubakaji wa Binti Waliotumwa na Afande Wakamatwa




Tovuti ya #MwananchiDigital imeripoti kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, kupitia Whatsapp amethibitisha kukamatwa kwa Wahusika katika Tukio la Binti aliyefanyiwa Ukatili wa Kingono na Vijana Watano
-
Kwa Mujibu wa Mwananchi, Waziri Masauni alitumiwa Ujumbe mfupi wa Maneno kupitia Mtandao wa #WhatsApp Agosti 6, kuulizwa iwapo watuhumiwa hao wameshakamatwa, ambapo alijibu kwa kuandika “tayari” ingawa hakufafanua zaidi
-
Agosti 4, 2024 Video ilisambaa Mtandaoni ikionesha Binti akifanyiwa ukatili wa Kingono na Vijana Watano, huku wakimtuhumu kwa kile kilichosikika katika video hiyo kuwa ametembea na Mume wa ‘Afande’ anayedaiwa kuwatuma Vijana hao kutekeleza Ukatili huo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad