Wimbo wa Diamond Platnumz Comasava Waingia Chat ya Billboard Marekani...



Wimbo wa msanii maarufu wa Tanzania, @diamondplatnumz, unaoitwa KOMASAVA umeandika historia kwa kuwa wimbo wa kwanza kutoka Tanzania kuingia kwenye chati za Billboard za Marekani.

Wimbo huo umeingia kwenye orodha ya Billboard U.S. Afrobeats Songs Top 50 na kushika nafasi ya 39 kama ingizo jipya. Hii ni chati ya muziki inayotolewa na Billboard, ikiorodhesha nyimbo za Afrobeats za wasanii wa Afrika zinazofanya vizuri zaidi nchini Marekani kwa kuzingatia mauzo, downloads, utazamaji wa video, na kusikiliza kwenye majukwaa ya muziki.

Diamond aliachia wimbo "Komasava" miezi mitatu iliyopita, akiwa na wasanii wa Afrika Kusini, Khalil Harisson na Chley, kisha Julai 26 mwaka huu, aliachia video ya remix ya wimbo huo akimshirikisha Jason Derulo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad