Yanga Kuanza Kurusha Karata yake ya Kwanza Ligi Kuu leo

Yanga Kuanza Kurusha Karata yake ya Kwanza Ligi Kuu leo




Bingwa wa Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga leo inaanza kampeni ya kutetea taji hilo ugenini dhidi ya Kagera Sugar.


Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.


Katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu timu hizo kukutana Mei 8 mwaka huu kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam Yanga ilishinda kwa bao 1-0.


Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo KMC itakuwa wenyeji Coastal Union kwenye uwanja wa KMC Complex, Kinondoni Dar es Salaam.


KMC na Coastal Union zilitoka suluhu katika mchezo wa mwisho wa Ligi kati ya timu hizo Mei 28 mwaka huu.


Kwenye uwanja wa Majaliwa, Lindi wenyeji Namungo itaikaribisha Fountain Gate.


Yanga, Coastal Union na Azam ambayo imecheza Agosti 28 dhidi ya JKT Tanzania zimechelewa kuanza ligi kutokana na majukumu ya kimataifa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad