Yanga yakataa bilioni 1.6 za Wydad kumng'oa Mzize

 

Yanga yakataa bilioni 1.6 za Wydad kumng'oa Mzize

Klabu ya Yanga imekataa ofa ya pili ya miamba ya soka nchini Morocco, Klabu ya Wydad Casablanca kiasi cha dola za Marekani 600,000 (sawa na zaidi ya Tsh 1.6 Billion) kwa ajili ya kunasa saini ya mshambuliaji kinda, Clement Mzize (22).


Ofa ya kwanza ya Wydad kwenda Yanga kwa ajili ya kuinasa saini ya Clement Mzize ilikuwa dola 100k (Tsh milioni 270) na kipengele cha kuongeza pesa hadi kufika Sh 400 million kutokana na performance yake uwanjani.


Chanzo kutoka ndani ya Yanga kimeeleza kuwa, uongozi wa klabu hiyo uliitupilia mbali ofa hiyo bila hata kuijadili. Wakawaambia Wydad wanataka Tsh 2.7 Billion ndipo wamuachie Mzize ambaye aliongeza mkataba mpya.


Wydad wamerejea na ofa ya Tsh 1.6 Billion, Yanga wamekataa. Klabu hiyo ya Morocco imepanga kuja na ofa mpya ya mwisho.


Kilichowavutia Wydad kwa Mzize ni eneo analocheza limekuwa gumu kupata washambuliaji bora wenye uwezo, hivyo wameona umhimu wa kumsajili Clement Mzize, pili umri wake ni mdogo lakini zaidi ni uwezo wake uwanjani hasa kwa siku za hivi karibuni.


Akiwa Afrika Kusini kocha wa Yanga SC, Gamondi alisema wana malengo ya kufanya vizuri katika ligi ya mabingwa hivyo mchezaji yoyote muhimu katika kikosi chao hataondoka labda yeye asiwepo.


Yanga watakataa ofa ya tatu ya Mwarabu aliyeenda kujipanga? Itakuwa maajabu!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad