AFANDE SELE: Azam TV Kuachana na Ngumi ni Ajali ya Kutisha

AFANDE SELE: Azam TV Kuachana na Ngumi ni Ajali ya Kutisha

AFANDE SELE: Azam TV Kuachana na Ngumi ni Ajali ya Kutisha

Legend @afandesele1976 ametoa maoni yake kuhusiana na sakata la Azam tv kujiondoa katika kurusha matangazo ya mchezo wa ngumi.


Afande ameandika

"Azam TV kuachana na mchezo wa ngumi,ni sawa na ajali ya kutisha kwa mchezo husika,na pia ni mkosi na hasara kubwa kwa mabondia,mapromota na mashabiki hasa sisi machizi ngumi ambao mchezo wa soka hasa soka la bongo na maigizo mengine sio mizuka yetu😴


Ni ukweli usiovaa nguo kwamba pamoja na Serekali kuwa na sera ya michezo inayoshughulikia michezo,lakini tayari serekali kupitia wizara husika imeonekana kufeli vibaya katika kusimamia na kuinua sekta ya michezo yote kiasi cha kukatisha ndoto na ajira za vijana wengi wenye vipaji,lakini ujio wa Azam TV umegeuka kuwa ukombozi kwa baadhi ya michezo kama mchezo wa ngumi ambao tayari ulikua umesahaulika kwa kukosa hamasa na mvuto kabisa ndani ya jamii✊


Sasa kwa kitendo cha Azam TV kupigana kibuti na mchezo wa ngumi kwasababu zozote zile ambazo kivyovyote haziwezi kuwa juu ya uwezo serekali,huku Serekali yenyewe kupitia wizara ikichukulia poa jambo hili kwa kutotimiza wajibu wake,basi maana yake serekali itakua imechangia moja kwa moja kupotea kwa ajira hizo nyingi za vijana wanaocheza mchezo wa ngumi,na kwasababu hizo wizara ya michezo itakua imepoteza uhalali wake kwa kwenda kinyume na sera ya nchi na ilani ya chama tawala chenye serekali hiyo juu ya kusimamia,kuinua na kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini.😎


Angalizo☝️

Tuokoe mchezo wa ngumi kwakua michezo ni ajira, na michezo ipo mingi hivyo serekali na wadau wache kutazama mchezo mmoja wa soka pekee,tena hata soka lenyewe isiwe kwa Simba na Yanga pekee au Taifa Staz ambapo huko pia viongozi wanaonekana kutafutia kick zaidi sio kuwa na mikakati endelevu ya kuinua soka letu,,ndio sababu hata ligi yetu ya soka imejaa maigizo ya ubabaisshaji na upangaji wa wazi wa matokeo ,kitu kinachosababisha ili kuwa chizi mpira kwa ligi ya bongo kunategemea na uwezo au uamuzi wako wa kufikiri vizuri na kujua tofaut ya uongo na ukweli,siasa na uhalisia,kinyume na hapo labda uwe mkamaria yaani mcheza kamari au betman

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad