Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob ameshindwa kupata dhamana leo September 26, 2024 baada ya Jopo la Mawakili wa Serikali kuwasilisha maombi mapya katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga alitarajia kutoa uamuzi juu ya maombi ya Serikali yaliyowasilishwa September 19, 2024 lakini kabla ya kutoa uamuzi huo Serikali imewasilisha maombi mengine ya kiapo cha ziada.
Kutokana na maombi hayo mapya, kesi hiyo imeahirishwa hadi October 01, 2024 ambapo Mahakama itatoa uaumuzi.
Itakumbukwa Jacob ambaye kada wa CHADEMA alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii.
Nje ya mahakama, Wakili wa utetezi Peter Kibatala amesema “Tumepinga vikali hoja za Serikali juu ya kiapo cha ziada kwamba Mahakama imesikiliza ushahidi kisha ikapanga hukumu na wewe unaleta tena Shahidi tukasema hapana hiyo sio sahihi, tunaamini uamuzi ungetolewa kama ulivyopangwa matokeo yangekuwa mazuri kwa Boniface, hivyo Mahamama kwa busara imeona itatoa uamuzi October 1,2024”