BOT YAPIGA MARUFUKU WAKOPESHAJI WA MTANDAONI KUTUMA MESEJI KWA WASIOHUSIKA

 

BOT YAPIGA MARUFUKU WAKOPESHAJI WA MTANDAONI KUTUMA MESEJI KWA WASIOHUSIKA

Baada ya Wadau mbalimbali kulalamikia vitendo vya udhalilishaji unaofanywa na Wakopeshaji Fedha kupitia 'App' za Mtandaoni, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa mwongozo unaopiga marufuku vitendo hivyo.


Mwongozo huo uliosainiwa Agosti 2024, unakuja katika kipindi ambapo kumekuwa na ongezeko la Taasisi mbalimbali za Ukopeshaji Fedha Mitandaoni ambapo baadhi zimelalamikiwa kuwaweka kwenye makundi ya WhatsApp Watu wa karibu wa Waliokopeshwa na kutuma Vitambulisho vyao.


Aidha, BoT imepiga marufuku Wakopeshaji Kutumia vitisho, vurugu au njia nyingine za kumuumiza aliyekopeshwa, Kutumia lugha za matusi kwa mteja au wadhamini wa mteja au namba nyingine kwenye simu yake kwa nia ya kumdhalilisha.


Pia, imezuia kuangalia na kuchukua Mawasiliano ya Watu wengine na kuwatumia meseji inapotokea mteja wao ameshindwa kulipa katika muda au asipolipa na Kutuma #TaarifaBinafsi za mteja katika mitandao kwa lengo la kumdhalilisha.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad