Dhamana ya Boni Yai Yagonga MWAMBA, Aendelea Kusota Rumande

 

Dhamana ya Boni Yai Yagonga MWAMBA, Aendelea Kusota Rumande

Wakati Jeshi la Polisi likikiri kumshikilia kada wa Chadema na mwanamitandao, Boniface Jacob maarufu ‘Boni Yai’, wakili wa chama hicho, Hekima Mwasipu amesema mteja wake amekosa dhamana.


Mwasipu amesema, Jacob anatuhumiwa kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo na sababu za kukosa dhamana jana Septemba 18, 2024 mlalamikaji ni makao makuu ya Polisi Dodoma, hivyo Polisi Mkoa wa Kinondoni ‘mikono yao imefungwa’.


“Tumeomba dhamana kwa bahati mbaya RCO Msangi (Davis Msangi)amesema yeye mikono yake imefungwa kwa sababu mlalamikaji ni makao makuu ya Polisi Dodoma, kwa mujibu wa sheria Polisi wanatakiwa kumshikilia sio zaidi ya saa 24 kwa kuwa alikamatwa saa kumi tarehe 18 tunatarajia mpaka leo hii saa 10 jioni saa 24 zitakuwa zimeshatimia, baada ya hapo tutachukua hatua za kisheria kuhakikisha Polisi wanalazimishwa kwa mujibu wa sheria kumpa dhamana,”amesema Mwasipu.


Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime katika taarifa aliyoitoa jana Septemba 18, 2024 alisema Jeshi hilo limemkamata na linamshikilia Jacob, mkazi wa Mbezi Msakuzi, jijini Dar es Salaam kutokana na makosa ya kijinai anayotuhumiwa nayo.


Boni Yai alikamatwa Septemba 18, akiwa maeneo ya Sinza, jijini Dar es Salaam, kwa mujibu wa wakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Hekima Mwasipu anayemwakilisha Jacob, ambaye ni kada wa chama hicho.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad