DIAMOND PLATNUMZ: NIMECHOKA KUMZAWADIA MAGARI ROMMY JONES

 

DIAMOND PLATNUMZ: NIMECHOKA KUMZAWADIA MAGARI ROMMY JONES

Mwimbaji maarufu wa Tanzania, Diamond Platinumz, amemzawadi kaka yake, Romeo Abdul Jones, nyumba mpya. Diamond alitoa zawadi hiyo wakati wa harusi ya Abdul, akieleza kwamba alitaka kumpa kitu kikubwa zaidi kama ishara ya upendo wake.


Diamond alisema kuwa Abdul alikuwa zaidi ya kaka kwake, na alistahili zawadi maalum. Alifafanua kuwa alikuwa amechoka kumpa magari ya kifahari, na hivyo akaamua kumpatia nyumba. Mwimbaji huyo aliongeza kuwa Abdul alikuwa na uhuru wa kuchagua nyumba anayoitaka, na angeinunua bila kusita.Pia alieleza kuwa kama Abdul angehitaji gari, angepewa bila tatizo.


"Nampenda sana kaka yangu.Najua ana uwezo wa kununua chochote anachotaka, lakini hii ni zawadi yangu kwake, nyumba. Nataka achague nyumba yoyote anayoipenda nami nitalipa.Nimechoka kumpa magari, lakini akihitaji gari pia nitampa.Kwa kaka yangu, hakuna jambo kubwa, kama hela zipo nitampa," Diamond alisema.


Hafla hiyo ilikuwa ya kufana, huku waimbaji na watu maarufu mbalimbali wakiwa wamehudhuria.Diamond aliandamana na Zuchu, mama yake, pamoja na dada zake, Esma Platinumz na Queen Darleen.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad