DIDY AKAMATWA KWA KOSA LA USAFIRISHAJI BINADAMU

DIDY AKAMATWA KWA KOSA LA USAFIRISHAJI BINADAMU


 Sean "Diddy" Combs, mfanyabiashara na msanii maarufu wa hip hop, amekamatwa jijini New York kutokana na mashitaka ya yanayohusiana na uchunguzi wa usafirishaji wa binadamu. Homeland Security ilimkamata Diddy mwenye miaka 54, kwenye hoteli ya Park Hyatt New York baada ya baraza la wazee wa mahakama kuidhinisha mashitaka yake.


Wakili wake, Marc Agnifilo, alisema Diddy amekuwa akitoa ushirikiano kwenye uchunguzi huo na anatarajia kusafisha jina lake mahakamani.


Tuhuma hizi zinajiri baada ya aliyekuwa mpenzi wake, Cassie Ventura, kumtuhumu kwa ubakaji na unyanyasaji wa kimwili, madai ambayo yalimalizwa kwa makubaliano yao binafsi. Diddy anakabiliwa na kesi kadhaa za unyanyasaji wa kijinsia na usafirishaji wa binadamu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad