DIVA THE BAWSE ATANGAZA KURUDI KWENYE UKRISTO, MAKANISA YAMKARIBISHA

Kwenye post yake ya leo kwenye instagram, mtangazaji Diva wa Wasafi FM, amethibitisha kuwa amepokea simu nyingi za pongezi kutoka kwa viongozi wa dini ya Kikristo baada ya kutangaza uamuzi wake wa kurudi kwenye Ukristo, ambako alilelewa tangu mwanzo. Kwenye ujumbe huo, Diva ameonyesha furaha na amani aliyopata kutokana na uamuzi wake, akieleza kuwa jamii ya Kikristo, ndani na nje ya nchi, imemkaribisha kwa upendo mwingi, amani, na furaha.

Anasema kuwa moyo wake una amani sana na familia yake pia imefurahishwa na uamuzi huo, hususan dada yake aliyeomba kwa muda mrefu Diva arudi kundini. Diva pia anasisitiza kuwa Yesu ni mwema kila wakati, na anaamini kuwa hakuna kitu kitakachoweza kuzuia baraka za Yesu, akihitimisha kwa maneno "If Jesus Say Yes, Nobody Can Say No!"("Yesu Akisema Ndio Hakuna Wa Kusema Hapana").

Uamuzi wa @divatheebawse kurudi kwenye imani yake ya Kanisa katoliki na safari yake yenye taarifa nyingi za kuwasaidia vijana kutoka kwenye hali mbalimbali, itakujia Hivi karibuni kwenye exclusive interview na @innolight_tz wa @SimuliziNaSauti!!... Usipange kukosa

Kwenye post yake ya leo kwenye instagram, mtangazaji Diva wa Wasafi FM, amethibitisha kuwa amepokea simu nyingi za pongezi kutoka kwa viongozi wa dini ya Kikristo baada ya kutangaza uamuzi wake wa kurudi kwenye Ukristo, ambako alilelewa tangu mwanzo. Kwenye ujumbe huo, Diva ameonyesha furaha na amani aliyopata kutokana na uamuzi wake, akieleza kuwa jamii ya Kikristo, ndani na nje ya nchi, imemkaribisha kwa upendo mwingi, amani, na furaha.

Anasema kuwa moyo wake una amani sana na familia yake pia imefurahishwa na uamuzi huo, hususan dada yake aliyeomba kwa muda mrefu Diva arudi kundini. Diva pia anasisitiza kuwa Yesu ni mwema kila wakati, na anaamini kuwa hakuna kitu kitakachoweza kuzuia baraka za Yesu, akihitimisha kwa maneno "If Jesus Say Yes, Nobody Can Say No!"("Yesu Akisema Ndio Hakuna Wa Kusema Hapana").

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad