Dk Nchimbi awataja Mbowe, Mnyika sakata la kibao

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amesema chama hicho hakiwezi kuvumilia matukio ya utekaji na uvunjifu wa amani na hakitakubali.


Mbali na hilo, Dk Nchimbi ametaka vyama vya upinzani ikiwemo Chadema kuungana pamoja kukemea, kukataa kufarakanishwa juu ya matukio ya utekaji na amepuuza taarifa za mitandaoni zinazolenga kuwahusisha viongozi wa Chadema na utekaji, mauaji.


Pia, CCM imelaani tukio la kutekwa na kuuawa kwa Mjumbe wa Sekeretarieti ya Chadema, Ali Kibao kikisisitiza hilo halikubaliki.


Kibao alitekwa Septemba 6, 2024 na watu wenye silaha eneo la Kibo Complex, Tegeta jijini Dar es Salaam akiwa kwenye basi la Tashriff akienda nyumbani kwake mkoani Tanga.


Mwili wake uliokotwa siku iliyofuata eneo la Ununio, Dar es Salaam ukiwa umeharibika na inaelezwa uso wake ulimwagiwa tindikali.


"Mtu yoyote anayehatarisha usalama wa raia, anayeteka raia au kikundi chochote kinachohatarisha usalama kinaharibu taswira ya CCM," amesema.


Dk Nchimbi amesema hayo leo Ijumaa, Septemba 13, 2024 alipozungumza na wahariri na waandishi wa habari, ofisi ndogo za CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.


Katika maelezo yake Dk Nchimbi amesema: "Tumemsikia Mwenyekiti wa Chadema, (Freeman) Mbowe akitoa mwelekeo wa chama chake kuwa kitachukua hatua. Nikiri Mbowe ni rafiki yangu, lakini Mbowe amefikishwa hapo na genge la utekaji?"


Dk Nchimbi amesema amekutana na Mbowe hivi karibuni katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi, Bakari Machumu: "Na Mbowe alinieleza juu ya suala la Kibao, kwa kumtazama Mbowe hahusiki na tukio hili la utekaji."


Pia, Dk Nchimbi amesema Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika:"Naye kwa kumwona tu, Mnyika hawezi kuhusika na utekaji."


"Chama chetu kimekasilishwa sana na matukio haya, tunataka uchunguzi wa haraka ufanyike," amesema.


Aanza mazungumzo na Chadema, ACT-Wazalendo


Dk Nchimbi amesema chama hicho kimeanza mazungumzo yasiyo rasmi na vyama vya upinzani vikiwemo Chadema na ACT-Wazalendo.


Mtendaji mkuu huyo amesema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa juu ya umuhimu wa mazungumzo baina ya CCM na vyama vingi, ili kudumisha kuaminiana na amani ya nchi.


Amesema kuna mazungumzo yasiyo rasmi yanaendelea na anayafanya yeye mwenyewe kwa lengo la kupata mwafaka wa Taifa.


"Mazungumzo ya Chadema nayaratibu mimi na ya ACT- Wazalendo ni makatibu wakuu wa vyama hivi. Muda ukifika tutawaeleza yakiwa rasmi," amesema.


Dk Nchimbi amesema hata washiriki wa mazungumzo hayo upande wa CCM watachagua wale wenye nia na lengo zuri la mazungumzo kwani baadhi "ukiwaona tu anavyozungumza unaona huyu hafai, tutachagua wenye lengo la maridhiano."


"Kwa upande wetu, tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha mazungumzo yanakuwapo," amesema Dk Nchimbi.Nchim

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad