Edo Kumwembe Aitisha Kikao Cha Dharura, Adai ni Upuuzi Kukataa Makipa wa Kigeni..




KIKAO CHA DHARURA. Nudgu zangu @shaffihdauda_ @jemedarisaid @geoff_lea @oscaroscarjr @georgeambangile @zakazakazi ...kwanini tuweke sheria ya kutokuwepo na makipa wa kigeni nchini? Sijui kwenu. Kwangu ni wazo la KIPUUZI. Kwamba tuna makipa wazawa bora sana na makipa wa kigeni wanatupotezea muda? Kwamba tuige kwa Waarabu. Tuna uhakika hawakuwa na makipa bora wazawa isipokuwa waliamua kulazimisha wazo tu? Kwamba tukiwahakikishia namba makipa wazawa bila ya ushindani wowote wataziimarisha klabu zetu? Kwamba tuwanyime wenye pesa zao wasipate kilicho bora langoni kwa sababu ya kanuni hiyo? Aishi alikaa miaka mingi langoni mechi kibao za kitaifa na za ndani hatukuwa na wasiwasi, alipangwa kwa uzawa au kwa ubora? Vijana washindane kwa ubora. Wakiondolewa wenye ushindani nadhani wataridhika zaidi. Kama Mwarabu aliweka hiyo kanuni ni kwa sababu alikuwa na products zilizo bora zaidi kuliko wageni. Yaani unikataze kula pilau kwa sababu Taifa lipandishe bei ya Mahindi? Na kwanini sio washambuliaji tupo kwa makipa? Mbona Mzize anacheza Musonda anakaa benchi? Mbona Asante Kwassi alimkimbia Tshabalala?
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad