Edo Kumwembe : Hakuna Mchezaji Kama Mbwana Samatta Hapa Tanzania



Kwa wenzetu mchezaji kama Mbwana Samatta ni lulu. Ni dhahabu. Alitufanya tuamini. Ametufanya tuamini. Amewafanya wengi waamini inawezekana. Inachosha kurudiarudia historia yake ya kutoka Mbagala hadi kucheza Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Inachosha kwa kweli.
.
Kifupi tu. Ni Mtanzania wa kwanza kuwa mfungaji bora Ligi ya mabingwa wa Afrika. Ni Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu ya Ubelgiji. Ni Mtanzania wa kwanza kuwa mfungaji bora huko. Ni Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na ni Mtanzania wa kwanza kufunga bao Ligi ya mabingwa Ulaya.
.
Ni Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi kuu England. Ni Mtanzania wa kwanza kuzifunga Liverpool na Manchester City. Ni Mtanzania wa kwanza kufunga bao Wembley na ni Mtanzania wa kwanza kufanya karibu kila kitu katika soka.
.
Wenzetu wanaheshimu watu waliofungua njia. Sawa, soka ni mchezo wa ukosoaji lakini wenzetu wanakosoa na kubakiza heshima kwa mtu kama Samatta. Niliona wazi kila siku Samatta anapoteza heshima yake. nilitamani astaafu. Mara nyingi huwa tunawaheshimu wachezaji wakubwa wakistaafu.

— Edo Kumwembe.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad