Edo Kumwembe 'Aziz K Anapoteza Sana Mipira Atazamwe Kwa Jicho la Pili'


Ndani ya uwanja pia Stephane Aziz Ki inabidi atazamwe kwa jicho jingine. Ni mtoto wa kishua. Mama yake ana kazi nzuri kule Afrika Magharibi. Wakati mwingine anaufanyia mpira masikhara mengi. Huwa tunamtazama Aziz katika matukio mazuri ya kuamua mechi. Hatumtazami namna anavyofanya masikhara na mpira. Anapoteza mipira ovyo.
.
Aziz anakosa ukomavu wa akili. Anawasaidia sana Yanga, lakini hapo hapo ni mchezaji anayepoteza mipira sana. Haonyeshi umakini mkubwa katika maeneo muhimu. Wakati mwingine anacheza kwa kile kitu Waingereza wanaita ‘mood’. Inategemea namna anavyojisikia kwa siku hiyo.

— Mchambuzi wa Mpira , Edo Kumwembe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad