Edo Kumwembe 'Kagoma ni Bonge la Mchezaji Alafu Mchezaji Kiburi'


Edo Kumwembe 'Kagoma ni Bonge la Mchezaji Alafu Mchezaji Kiburi'
Kuna Yusuf Kagoma. Bonge la mchezaji. Wakati Simba walipokuwa wanampigania Lameck Lawi kati yao na Coastal Union nilisafiri na Kagoma na Lawi kwenda Indonesia katika mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars dhidi ya Indonesia. Niliona sababu zote za Simba kumuwania Kagoma na siyo Lawi.
.
Kagoma ni mtu na nusu. Lawi alionekana kutetemeka katika mechi ya kawaida ambayo haikuwa na presha kubwa. Kagoma alicheza kama vile nilivyokuwa namuona Singida Fountain Gate. Anajua mpira halafu msela. Ana ‘kiburi’. Napenda wachezaji vizuri. Kiburi chanya. Mpira huwa hauwashindi. Kinachowashinda ni pale kiburi cha nje ya uwanja kinapozidi.
.
Kagoma ni mchezaji wa aina hii. Wale wachezaji ambao achilia mbali kujua mpira, lakini wanacheza huku mioyo yao ikiwa na inaongea ikisema “nyie wote wajinga mimi najua mpira”. Kuna faida ya kuwa na kiburi chanya. Katika uwanja uliosheheni chuki kama ule wa juzi ulimhitaji sana mchezaji kama yeye ndiyo maana Kagoma hakuyumba. Akili yangu iko palepale. Taifa Stars. Hawa ndio wachezaji wakutusaidia mbele ya safari. Kwanini inakuwa bora zaidi wakicheza timu hizi kubwa kama Simba na Yanga? Kwa sababu wanacheza mechi nyingi za kimataifa katika klabu zao. Inatusaidia.“

— Legend, Edo Kumwembe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad