GAMBIA YAONGOZA KWA UTALII WA KINGONO AFRIKA


Imeelezwa kuwa mpaka sasa Gambia ndilo taifa linaloongoza kwa utalii wa ngono barani Afrika. Na Ulaya wanaita kivutio kikuu barani Afrika kwa utalii wa ngono kwa wanawake.

Yaani 'pisi mikweche' za Ulaya, ambazo kilometa zake za umri zimesoma sana. Kimbilio lao ni Afrika Magharibi katika taifa hilo la Gambia. Ambalo vijana wake hutoa huduma kwa vizee hivyo vya kizungu.

Wanawake wengi ambao ni 'eji goo'. Waliostaafu kwenye mataifa kama Uingereza na kwengineko barani Ulaya. Wanapendelea sana kutembelea huko nchini Gambia.

Hawaendi kushangaa chui, sokwe, tumbili wala pofu kama wale wa Tarangire. Bali wanaenda kutafuta vijana shababi wa kiume, ama kwa ajili ya uchumba au kwa ngono tu za kulipana.

Wakati tumezoea kusikia vijana wengi wa Afrika Magharibi. Wakikimbilia Ulaya kucheza soka au Marekani kubeba boksi. Vijana wa Gambia wao wanajali uzalendo wa kubaki nyumbani kwao na kuhudumia wageni wa kike kingono.

Wavulana na wanaume hao, hujulikana kama 'bumsters'. Na jukumu lao kubwa la kila siku iendayo kwa Mungu, ni kuhudumia hao wageni wa kike. Ambao kimsingi ni jua la jiiooooni kiumri.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad