Golikipa wa Mamelodi Sundowns Aweka Rekodi Tuzo za Ballon Dor


Nyanda wa Mamelodi Sundowns na timu ya Taifa ya Afrika Kusini Ronwen Williams ameweka rekodi ya golikipa wa kwanza anayechezea klabu ya Afrika kujumuishwa kwenye orodha ya magolikipa wanaowania tuzo ya Ballon d’Or ya golikipa bora wa mwaka (Yachine Trophy).

Waandaaji wa tuzo hiyo ya Ufaransa wametoa orodha ya magolikipa wanaowamia tuzo hiyo ambao pamoja na Diogo Costa, Gianluigi Donnarumma, Gregor Kobel, Andrei Lounine, Mike Maignan, Giorgi Mamardachvili, Emiliano Martinez, Unai Simon, Yann Sommer na Ronwen Williams.

Williams ambaye alichaguliwa kuwa golikipa bora kwenye michuano ya AFCON 2023 baada ya kucheza mechi nne bila kuruhusu bao (clean sheets) na kuiongoza Afrika Kusini kumaliza nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo.

Williams alikuwa na ‘Clean Sheets’ 35 kwenye michezo 59 kwenye msimu wa 2023-24 akiiongoza Mamelodi Sundowns kutwaa ubingwa wa African Football League pamoja na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad