Erling Haaland, mchezaji wa Manchester City, ameweka rekodi sawa na Cristiano Ronaldo kwa kufikisha magoli 100 akiwa na klabu moja ndani ya mechi 105 alizocheza. Ronaldo alifikisha rekodi hiyo akiwa na Real Madrid, pia kwa mechi 105.
Haaland ameonyesha wazi kuvutiwa na Ronaldo, akimtaja kama mchezaji wake anayemuenzi. Akiwa amejifunza mengi kutoka kwa staa huyo wa zamani wa Real Madrid, Haaland amesema, "Mara nyingi humtazama Ronaldo kupitia YouTube, nikijifunza jinsi anavyocheza ndani ya boksi, akifanya miondoko miwili au mitatu kabla ya kushambulia."
Uwezo wa Haaland katika kufunga magoli unaashiria ushindani mkali, na huenda akatwaa tuzo ya Ballon d'Or kutokana na uwezo wake wa kipekee wa kufumania nyavu.