Baada ya kuachana na benchi lao zima la ufundi lililokuwa linaongozwa na Yousouph Dabo, Azam FC leo imemtangaza Rachid Taoussi (65) Raia wa Morocco kuwa Kocha wao Mkuu mpya.
Kocha Rachid amekuja na benchi lake zima la ufundi kuanzia Msaidizi, Kocha wa viungo hadi Kocha wa Magolikipa.
“Tunayo furaha kumtangaza, Rachid Taoussi, kuwa Kocha Mkuu wetu mpya kwa mkataba wa mwaka mmoja,Taoussi amekuja na wasaidizi wake watatu, Kocha msaidizi, Ouajou Driss, Kocha wa utimamu wa mwili, Badr Eddine na Kocha wa makipa, Rachid El Mekkaoui”
Kocha Rachid ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 kwenye kazi ya Ukocha na amewahi kufundisha timu za FAR Rabat, Wydad, Berkane, Raja Casablanca zote za Morocco na ES Setif na CR Belouzdad za Algeria.