Huyu Ndiye Aliyejaribu Kumpiga Risasi Trump, Alihamasisha Vita Ukraine

Huyu Ndiye Aliyejaribu Kumpiga Risasi Trump, Alihamasisha Vita Ukraine


Baada ya kusambaa kwa taarifa za kujaribu kumshambulia kwa risasi mgombea wa urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump, mtuhumiwa Ryan Routh anayetajwa kuhusika na tukio hilo aliwahi kuhamasisha vita huko Ukraine.


Hii ni mara ya pili kwa Trump kunusurika kifo kwenye mashambulio ya risasi katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi, kwani wiki tisa zimepita tangu Julai 13, 2024 alipokumbana na tukio kama hilo wakati akihutubia huko Butler.


Routh alidaiwa kutenda tukio hilo jana Jumapili Septemba 15, 2024, akimlenga Trump aliyekuwa akicheza Golf kwenye uwanja wake wa Golf wa kimataifa uliopo West Palm Beach.


Reauters iliripoti Routh alishtukiwa mapema na walinzi wa Trump kabla hajaleta madhara na alikimbia kabla ya kukamatwa. Baada ya tukio hilo, Trump kupitia ofisi yake binafsi alitoa taarifa kwa umma kuwa yupo salama.


“Kuna risasi zilipigwa karibu na eneo nilipokuwa, lakini kabla ya uvumi kusambaa nataka kuwafahamisha nipo salama na mzima, hakuna kitachonipunguza kasi," amesema Trump ambaye yupo kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais na Kamala Harris wa Democratic.


Kwa mujibu wa Reuters, mtuhumiwa Ryan Routh ambaye ametambuliwa na mashirika ya habari, huku Shirika la Ujasusi la nchi hiyo (FBI) likichunguza jaribio hilo la mauaji lililofanyika Florida, aliwahi kuonekana kwenye mkutano wa kuunga mkono Ukraine, katika uwanja wa Uhuru mjini Kyiv, Mei 29, 2022.


Routh, alikaa mjini Kyiv mwaka 2022 ili kuhamasisha watu kupigana kwa ajili ya Ukraine, alipohojiwa na vyombo vya habari alisema lengo lake la awali lilikuwa kupigana kwa ajili ya nchi hiyo, badala yake alihamasisha wengine kupigana.


"Vita vingi ni vya kivuli, lakini vita hivi hakika ni nyeusi na nyeupe ni kuhusu mema dhidi ya mabaya," amesema Routh katika mahojiano yaliyochapishwa na Newsweek Romania Juni 2022.


Lakini, miezi minne baada ya uvamizi kamili wa Russia nchini Ukraine, Routh aliamua kuomba msaada wa kimataifa zaidi na alipoulizwa kuhusu alichokuwa akifanya alisema lengo lake la awali lilikuwa kupigana, lakini baada ya mpango huo kutofanikiwa, kwa sababu umri wake na ukosefu wa uzoefu wa kijeshi vilimfanya asikubaliwe, aligeukia kuhamasisha kwa wengine.


Routh pia alikiambia chombo cha habari cha Semafor Machi, 2023 kwamba amekuwa akijaribu kuajiri wapiganaji wa Afghanistan waliofunzwa na Marekani kupigania Ukraine dhidi ya Urusi, lakini wizara ya ulinzi mjini Kyiv haikukubali kuwapa viza.


Tangu jana Jumapili, vyombo vya habari vya New York Times, Reuters na Fox News vimemtaja, Routh (58) kuhusika na tukio la kujaribu kumpiga risasi Trump, Rais wa zamani wa Marekani.


Rekodi zaidi zinamtaja Routh kuwahi kuishi North Carolina kwa sehemu kubwa ya maisha yake kabla ya kuhamia Hawaii, mwaka 2018. Huko Hawaii, yeye na mwanaye walionekana kuendesha kampuni ya mabanda.


Pia kwa rekodi za wapigakura zinaonyesha alijiandikisha kama mpigakura asiyeegemea upande wowote North Carolina mwaka 2012, na kupiga kura kwa mara ya mwisho kwa mkono katika uchaguzi wa awali wa chama cha Kidemokrasia wa jimbo hilo Machi 2024.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad