KARDASHIAN: KILA MTU ALIKUWA UCHI KWENYE PART ZA DIDDY

KARDASHIAN: KILA MTU ALIKUWA UCHI KWENYE PART ZA DIDDY

KARDASHIAN: KILA MTU ALIKUWA UCHI KWENYE PART ZA DIDDY

Khloé Kardashian amezungumzia sherehe za Sean “Diddy” Combs kwenye kipande cha episode ya “Keeping Up With the Kardashians” kilichoibuliwa baada ya msanii huyo kukamatwa kwa tuhuma za usafirishaji wa watu kwa ajili ya kuwatumikisha kingono.


Mwanamitindo huyo, mwenye umri wa miaka 40, alikumbushia kuhudhuria moja ya sherehe za kifahari za Diddy kwenye kipindi hicho kilichorushwa Agosti 17, 2014. Khloé aliwaambia dada yake Kourtney Kardashian na rafiki yao Khadijah Haqq kuwa sherehe hiyo ilikuwa na watu wengi waliokuwa hawajavaa nguo.


Sherehe za Diddy zilikuwa maarufu kwa kuvutia mastaa wengi kama vile Justin Bieber, French Montana, na Quincy Combs. Khloé alielezea kuwa hakuweza kulala baada ya kuhudhuria sherehe hiyo iliyofanyika hadi alfajiri, akiongeza kuwa Kourtney angefurahia kuona watu wakivua nguo.


Wiki iliyopita, Diddy, mwenye umri wa miaka 54, alikamatwa New York na kufunguliwa mashtaka ya kula njama, usafirishaji wa watu kwa njia ya udanganyifu, na usafirishaji kwa ajili ya ukahaba. Mashtaka hayo yanadai kuwa msanii huyo aliendesha biashara haramu kwa muda mrefu ili kutimiza matakwa yake ya kingono na kuficha matendo yake.


Wakili wa Diddy alisema kuwa mashtaka hayo si ya haki na wanamvunja moyo kutokana na hatua ya ofisi ya mwendesha mashtaka kuendelea na kesi hiyo. Hii si mara ya kwanza Diddy kukumbwa na tuhuma kama hizo, kwani mwaka 2023, mpenzi wake wa zamani, Cassie Ventura, alimshtaki kwa madai ya ubakaji na unyanyasaji wa kimwili, ingawa walifikia makubaliano.


Diddy sasa anakabiliwa na mashtaka mengine kutoka kwa wanawake wengi, ikiwa ni pamoja na Dawn Richard, aliyedai kuwa alishuhudia unyanyasaji wa kimwili dhidi ya Cassie wakati walipokuwa wakifanya kazi pamoja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad