Kimenuka...Safari za Mabasi ya Katarama Zasitishwa

 

Kimenuka...Safari za Mabasi ya Katarama Zasitishwa

Mamlaka ya Uthibiti Usafiri Ardhini LATRA imesitisha leseni ya safari ya mabasi ya kampuni ya Katarama kwa kosa la kuchezea mifumo ya mwenendo ya mabasi yaliwekwa na Latra kwenye mabasi hayo ambayo kusitishwa kwake safari yanaanza kesho.


Hayo ameyasema Leo Mkurugenzi wa Latra Habibu Suluo wakati alipokutana na wamiliki wa mabasi ya BM Coach,Super Feo,Abood Bus na Katarama Bus jijini Dar-es-salaam.


Habibu amesema Kampuni ya Bm Coach , Super Feo na Abood Bus imepewa wiki moja wamiliki wa mabasi hayo yanayofanya safari za mchana na usiku kubadilika kutokana na ajali zinazotokea siku za nyuma kwenye mabasi hayo.


ACP Nassoro Sisiwayah Mkuu wa Operesheni kikosi cha usalama Barabarani (T)amesema watafuatilia waliochezea mfumo huo wa LATRA ili kubaini wahalifu na kupelekwa mahakamani.


Kwa upande wake Omary Msigwa Mmiliki wa Mabasi ya Super Feo amesema watafuata sheria na kanuni za barabarani.


Nae Abdala Kiongozi Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa mabasi TABOA ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mabasi kuzingatia sheria na kanuni za Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini LATRA .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad