KIPA AYOUB LAKRED KUMPISHA ELIE MPANZU SIMBA

 

KIPA AYOUB LAKRED KUMPISHA ELIE MPANZU SIMBA

Simba Sc kumtema kipa Ayoub Lakred ambaye kama atakuwa hajapona mpaka dirisha dogo linafunguliwa Desemba.


Simba haitakuwa na nafasi ya kujiuliza sana kwa Lakred wakati huu ambao Moussa Camara akiwa ameanza kwa moto mkali ndani ya timu hiyo akifanya mageuzi makubwa ndani ya kikosi hicho.


Nyuma ya Camara kuna Aishi Manula ambaye licha ya kurudi kwa kishindo lakini bado amelazimika kusubiri nafasi yake ikichukuliwa na kipa huyo raia wa Guinea.


Mbali na Lakred raia wa Morocco, mtu wa pili ambaye anaweza kupisha ni Mkongomani Fabrice Ngoma ambaye amepoteza nafasi kabisa kikosi cha kwanza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad