KOCHA GAMONDI : NINA WACHEZAJI WAKUBWA KULIKO CBE

KOCHA GAMONDI : NINA WACHEZAJI WAKUBWA KULIKO CBE


Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kikosi chake kina Wachezaji wakubwa ambao wanaweza kufanya jambo bora kuliko Wapinzani wao CBE ya Ethiopia ambao wanacheza nao mchezo wao wa marudiano kesho September 21,2024 Uwanja wa New Amaan Complex, Visiwani Zanzibar ambapo amesema anaamini watafanya jambo bora kuliko Wapinzani.


Akiongea leo Gamond amesema “Mechi iliyopita kweli tulikosa nafasi nyingi lakini kama Kocha kukosa nafasi hutokea, muhimu ni kuwa na timu yenye uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi, ukweli ni kwamba lazima kesho tutumie nafasi tunazopata, sitaki kuwapa Wachezaji wangu presha kisa tulikosa nafasi nyingi, najua watacheza kwa utulivu lakini muhimu ni kuhakikisha tunatumia nafasi tunazopata”


“Hali ya Wachezaji wangu ni nzuri, tumejiandaa vizuri sana na tumepata muda wa kujiandaa, nina Wachezaji wakubwa sana ambao wanaweza kufanya jambo bora kuliko Wapinzani wetu, najua Wachezaji wangu wanafahamu umuhimu wa kufuzu hatua ya makundi #CAFL” —— Gamond


Kwa upande wake, Ibrahim Bacca amesema “Hapo awali nilikuwa naangalia mpira wa ligi ya mabingwa kwenye TV, leo hii Watu wanakuja kunitazama Mimi, ninafarijika sana na kuona nina jukumu zito la kuhakikisha naisaidia Yanga kufikia malengo yake”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad