Lissu: Vyombo vya Usalama Haviwezi Kujichunguza, Vichunguzwe na Kusafishwa

Lissu: Vyombo vya Usalama Haviwezi Kujichunguza, Vichunguzwe na Kusafishwa


Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema haiwezekani Vyombo vya Usalama nchini kuchunguza Matukio ya Uhalifu ikiwemo Utekaji na Mauaji yanayoripotiwa nchini kwasababu vinatuhumiwa kuhusika na matukio hayo.


Akizungumza na JamboTV, Lissu amesema hayo leo Septembea 11,2024 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Saalam baada ya kuwasili kutoka Ubelgji.


Lissu amesema Jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa hawawezi kujichunguza kuhusu matukio ya utekaji na mauaji yanayoendelea nchini, badala yake kinatakiwa chombo kingine kiundwe au kitoke nje ya nchi kwa ajili ya kuwachunguza.


“Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa ambayo sasa anaiongoza mwenyewe (Rais Samia), hivyo ndio Watuhumiwa wa kwanza, watajichunguzaje?, lini Jeshi na Polisi na Usalama wa Taifa waliwahi kuchunguza chochote cha mambo haya!?, kwahiyo kutuambia Vyombo vya Usalama vichunguze, haviwezi vikajichunguza vyenyewe, Vyombo vya Usalama vinahitaji kuchunguzwa, kusafishwa kuhakikisha hakuna majambazi waliovaa 'uniform' na wanaolipwa Mshahara wa umma.


“Kuna taratibu zinazojulikana za Kimataifa za kuweza kuchunguza haya, utaratibu wa kawaida kabisa huwa ni Tume ya Kijaji ya Uchunguzi, sasa tatizo la Tume ya aina hiyo kwa kwetu ni kwamba inaripoti kwa Rais na taarifa yake inakuwa siri, kwahiyo huko sio pakwenda.


“Pakwenda namna pekee na halali ya kuchunguza hili ni kuleta uchunguzi wa Kimataifa, tulete kama walivyofanya jirani zetu wa Kenya miaka fulani miaka ya MOI, walikuwa wanauaua Watu hivihivi, utekaji hivihivi, walileta Wachunguzi, Wapelelezi kutoka Scotland Yard na kwetu kwa wenye kumbukumbu kama Mimi nakumbuka lilipoungua jengo la Benki Kuu mwaka fulani walileta Wapelelezi kutoka nje.


"Kwa hiyo kwenye hili ambalo Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyenyewe ndio Watuhumiwa wa kwanza inabidi wachunguzwe na Watu wanaoaminika na sio wajichunguze wao huko tutakuwa tunadanganyana,” amesema Tundu Lissu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad