Mavoko Atakaa Ushikaji na Diamond, Ile WCB ilikuwa Biashara Yaliisha


Staa wa Bongofleva mwenye skills za ‘Messi’ na spirit za ‘Bilionea Kid’ Rich Mavoko ( @richmavoko ) ambaye mida hii anasumbua mitaa na goma lake jipya la ‘kill my self’ ft. Chinno, amesema hajawa na mawasiliano kwa muda mrefu na President wa WCB @DiamondPlatnumz toka walipomaliza kufanya biashara.

“Hatujawahi kuwa Washkaji tulikuwa tunafanya biashara baada ya biashara kuisha basi ambacho unakiona ndio inatakiwa kiwe hivyo, mimi niko Real na yeye yuko Real so biashara yetu ambayo imetukutanisha imeisha basi kila Mtu anafanya vitu vyake vya kimaisha mambo mengine yanaendelea” ——— Mavoko.

Kuhusu uhusiano wake na Wakali wenzake waliokuwa pamoja WCB ambao ni Rayvanny na Harmonize, Mavoko ametiririka yafuatayo ——— > “Ndio hivyo tumekutana kazini sisi ni Watoto wa kiume, hatuwezi kunununiana tunaongea tunasalimiana ... hata tukikutana leo kesho tunasalimiana tunaongea lakini kusema eti tulikuwa na ushkaji kinomanoma wa kukujua leo wewe una changamoto gani hapana, ni vile tumekutana ofisini love ya ofisini, Mfanyakazi mwenzako.... ilikua iko hivyo”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad