MBOWE: KWETU HUU NI MWEZI WA MAOMBOLEZO

 

Mbowe


“Tunatamani Taifa hili liongozwe kwa Katiba iliyo bora ambayo itazaa sheria iliyo bora na vyote kwa pamoja vitatengeneza ustawi ulio bora kwa Raia wote, kwa muda mrefu katika Nchini yetu kumekuwa na utamaduni wa waliopo katika madaraka kuamini utashi wa Kiongozi Mkuu ndio unapaswa kuwa dira ya Taifa, haipaswi kuwa hivi”


“Sisi katika Chama chetu (CHADEMA), kwetu huu ni mwezi wa maombolezo, tunawashukuru Watanzania wote wa Vyama vyote, Taasisi mbalimbali, Watu binafsi ambao wamelia na sisi, kwetu umekuwa ni mwezi mgumu mno, na ndio sababu nilisema katika hatua za kwanza, tunapata wakati mgumu kutafakari namna ya kuufanya wajibu ulio bora ndani ya TCD (Kituo cha Demokrasia Tanzania), wakati huo tukilia kwa madhila tunayoyapata”


“Ili demokrasia iwe na maana lazima wakati wote itambue haki, lazima pawe na utashi wa kisiasa na utashi huu wa kisiasa utoke zaidi kwa wale waliopoewa dhamana ya kuongoza Taifa letu”


“Nimesema kwetu ni mwezi wa majonzi kwa sababu tunapoizungumza demokrasia na haki ya kuishi, haki kwa Watu wote, basi iwe kwetu sote, na sio katika kikundi fulani cha Watu wawe ni Watu wa kulia, Watu wa kuomboleza, nimesema Ndugu zangu huu kwetu ni mwezi mgumu kwasababu tumewapoteza wenzetu na tunaendelea kutokujua wenzetu wako wapi, Watumishi wenzetu katika wajibu wa siasa ambao katika mazingira ya kutatanisha wamepotea katika uso wa dunia, ama pengine niseme wamepotea katika macho ya Watu, kama wapo katika macho ya Vyombo vingine! hatujui” —— Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiongea katika Mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) leo September 19, 2024 Jijini Dar es salaam unaojadili hali ya demokrasia Nchini ambapo Mbowe kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa TCD

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad