MREMBO HUDDAH AMUOMBA MSAMAHA MBUNGE

MREMBO HUDDAH AMUOMBA MSAMAHA MBUNGE

MREMBO HUDDAH AMUOMBA MSAMAHA MBUNGE

Mkali wa maudhui ya mitandanoni kutoka Kenya, Huddah Monroe ameomba msamaha kwa Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya.


Wawili hao walihusika katika vita vya maneno mtandaoni baada ya Huddah kutaja Sh10,000 alizotumiwa na mbunge huyo kwamba hakutambua kwa kuwa watu wengi walimtumia fedha nyingi zaidi.


“Nakuheshimu sana Peter Salasya na naomba radhi kwa kukuweka mtandani, tukutane kileleni, ubarikiwe. Sina chochote dhidi yako Peter Salasya. Bado nina heshima kubwa kwako na upendo mwingi. Wewe ni mtu mkubwa. Jitunze. Hakuna binadamu aliye na mipaka.


Huddah pia alifafanua kuwa hajawahi kukutana na Salasya.


“Kwa njia, hatukuwahi kukutana. Ilianza kwenye mitandano na kuishia hapa.”


Huddah alisema kuwa bado yuko single na anachumbiana na kila mtu kabla ya kumpata Mr Right wake.


“Bado nipo single nachumbiana na kila mtu kabla sijapata mpendwa wangu Mr Riht wangu, na aliye bora ndiye ashinde,” aliandika Huddah.


Awali mbunge huyo alidai kuombwa Ksh 10,000 na Huddah ndipo akamtumia lakini mapokeo ya Huddah yalikuwa ya kumchafua wakati aliomba mwenyewe.


“Huyu jamaa alinitumia Ksh 10,000 ambazo hata sikuziona. Coz natoa zawadi ya Sh 50,000. Mimi si wakienyeji bro. Tafuta size yako,” aliandika Huddah katika ukurasa wake wa Instagram.


Aliongeza kuwa hakuona tarifa ya kuingia kwa fedha hizo kutoka kwa mbunge, “Ningeonaje Ksh 10,000 hakika, wakati watu wananitumia Ksh 2,200,000.


“Usiniharibie jina cause of 80 dollars bro. Wacha members wajue nilirudisha chakula cha kuku,” aliandika Huddah kabla ya kuomba msamaha kwa alichokifanya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad