MWANAMUZIKI TYLA ADAIWA KUPANDIKIZWA KUUA MUZIKI WA AFROBEAT KUTOKA NIGERIA...



Tyla ghafla amegeuka a mega superstar. Undeniably so, wimbo wake wa “Water” umeenda duniani. Ila sasa watu wana mashaka, ulienda organically au tumelazimishiwa?

Ila siku hizi kuna organic breakthrough kweli, ikiwa lengo ni kwenda viral, na nyenzo ni tiktok na mchawi ni “investment money”? Siku hizi a Hit Song haihitaji a well written song, bali a viral moment na pesa.

Why wanasema ni industry plant? Ukiondoa kuibuka ghafla, ni fact kwamba amekuwa anashinda Awards kubwa zote tena mbele ya watu ambao one can argue wamepiga vitu vikubwa zaidi yake. Kuanzia Grammys, hadi hii juzi MTV.

Ile Grammys wa Nigeria wali-mind ila wakauchubua kiaina. Artist like Davido wali feel kama wametumika ku-push agenda ila zawadi akapewa mwingine. Sasa hii ya juzi Category ilikuwa inaitwa “Afrobeats Artist of the Year” na Tyla akiwemo alongside Naija Artists. Ameshinda, na alivyofika kutoa speech akasema lakini yeye anafanya Amapiano, alafu akawa congratulate Nominees wengine.

Kabla hata Wanaija hawajasema kitu, Wamarekani wakaanza kusema. Joe Budden (Rapper/Podcaster) amedai “She is an Industry Plant”. Reason why americans wanaanza kuhisi hivyo, ni sababu Artists like Burna Boy, Wizkid, Davido, Asake, wanaupiga mwingi mno huko USA, sio shows, interviews, streams, etc ila Tuzo anachukua mwingine.

Record Labels kubwa (Sony, Warner, Universal) zimekuja Africa, na zimekuwa zinataka kuwa “INCLUSIVE”. Ila badala ya kujifunza kuwa sio kila Nchi/Artist wanafanya Afrobeats, wao wameamua kutuweka wote kwenye box moja, kitu ambacho kinaleta madhara sasa.

Je is this an opportunity ya BONGOFLAVA nayo kupaza sauti, isikike ili wakianza kurekebisha makosa na sisi tuhesabiwe? Je tunaweza kuwa na Sauti ikiwa hatuna DEFINITIVE IDENTITY? Kumbuka sasa hivi Bongoflava ni mixture ya Amapiano na Afrobeats?

It will be interesting to see what transpires; Nigeria watasusia hizi tuzo (maana wanatumika)? Je ndio sisi tutapata upenyo? Je tunaweza toboa ikiwa tunawekwa kundi moja? Unadhani TYLA anastahili ushindi au kweli kuna kitu nyuma ya pazia? let’s discuss

The Leader

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad