Mzize Afunguka Utamu na Maajabu yake Kila Akianzia Bench Akiwa na Yanga.....

 

Mzize Afunguka Utamu na Maajabu yake Kila Akianzia Bench Akiwa na Yanga.....

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Clement Mzize ameweka wazi kuwa akitokea benchi huwa anafanya vizuri zaidi kuliko anapoanza ndani ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo .

Amesema mara nyingi anapokuwa benchi huwa anaangalia mapungufu ya mabeki wa timu pinzani na kuingia kuwaadhibu kwa kufunga au kuwasumbua wapinzani.

Mzize amesema akianzia benchi huwa anausoma vizuri mchezo na kuingia kusahihisha makosa ya wenzake anapoingia uwanjani.

Amesema mwaka huu nimekuja kivingine akili imekuwa tofauti na msimu uliopita, kwa kuwa akili ilikuwa ya kitoto na kuathiriwa na maneno ya mashabiki mtandaoni.

“Nikianzia benchi na kuingia kuchukuwa nafasi ya mtu nakuwa wa moto zaidi, mguu wa kulia upo vizuri lakini kushoto ni zaidi na ndio naweza kudribo.

“Nikicheza pembeni inakuwa nzuri sababu akili yangu kufunga zaidi hasa nikicheza namba saba ni rahisi kwa kuwa natumia kushoto,” amesema Mzize.

Kuhusu ushindani wa namba, Mzize amesema kwa anahitaji kupamabana na kuonyesha kitu kwa kocha Miguel Gamondi ili kumuamini na kumpa nafasi.

Mzize ametoka kuaminika na kocha Gamondi lakini pia kutajwa kutakiwa na klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco ambao wanatajwa kuweka dau ili kupata hutuma ya mshambuliaji huyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad