Nayce Moshi 'Gari Yanga IST Nimenunua Kwa Pesa Yangu Sijahongwa'





Mhudumu wa Basi @naycemoshi kupitia Interview yake amefunguka kuwa i bali ameinunua kwa juhudi zake mwenyewe.


Nayce ameeleza kwamba amenunua Gari hiyo Milioni 17.5 ikiwa mpya kabisa na kwa sasa inafanya Shughuli ya Bolt ambapo kila siku anaingiza pesa na Mungu akijalia ataongeza Gari nyingine kwa ajili ya Bolt.

Hivi karibuni Nayce Moshi amezawadiwa Iphone 15 na Bosi wake kutokana na mchango wake wa kuitangaza vyema biashara yake ya Mabasi.

Nayce Moshi amedokeza kuwa hajali watu wanaoponda kuhusu kimo, umbo na tumbo lake kwani yeye ni Mchaga hivyo anajikubali kwa namna yoyote ile alivyo.

Nayce Moshi hivi sasa ana umri wa miaka 21, alipata umaarufu mkubwa mwaka jana baada ya kuwa anaji-post kwenye mitandao ya kijamii akifanya kazi ya uhudumu wa Basi, mwanzoni ilikuwa vigumu kwani wenzake walikuwa wanamuona kama anajidhalilisha kutokana na jamii kudharau baadhi ya kazi lakini baada ya umaarufu na kuanza kupata dili mbalimbali hivi sasa Wahudumu wengi wa Mabasi hufata nyayo za Nayce na wao pia wanatamani kujulikana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad