OFFSET AMSHUTUMU CARD B KUMSALITI AKIWA MJAMZITO

OFFSET AMSHUTUMU CARD B KUMSALITI AKIWA MJAMZITO

OFFSET AMSHUTUMU CARD B KUMSALITI AKIWA MJAMZITO

Mahusiano kati ya Cardi B na Offset yamekuwa na misukosuko mingi, kutokana na tuhuma za usaliti. Mgogoro wao ulioibuka jana usiku umechukua sura mpya, ambapo Offset anamshutumu Cardi kwa kumsaliti akiwa mjamzito, jambo ambalo liliibua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii. Offset alikomenti kupitia akaunti yake ya Instagram akimtaka Cardi kusema ukweli juu ya madai hayo, ambayo Cardi alikiri kwa hasira kupitia tweet yake iliyosema, “AND DID!!!!!!”


Baada ya shutuma hizo, Cardi B alijibu kwa kufoka kupitia Instagram Live, akieleza ambavyo Offset amekuwa akijaribu kumshawishi kwa zawadi na vitisho ili warudiane. Huku akiendelea na mchakato wa talaka, Cardi alifunguka zaidi juu ya ugumu wa kuvumilia vitendo vya Offset. Hata hivyo, licha ya uvumi wa usaliti kuwa chanzo kikuu cha mgawanyiko wao, vyanzo vya karibu vinaeleza kuwa usaliti haukuwa sababu pekee ya Cardi kuomba talaka.


Uhusiano wa Cardi B na Offset, ambao ulianza kwa siri mwaka 2017, umekuwa ukizungumziwa sana kutokana na drama na skoendo zinazowahusu. Mwaka 2020, Cardi B aliomba talaka kwa mara ya kwanza lakini walirudiana baada ya muda mfupi, wakidai wamekuwa imara zaidi. Wanandoa hao wana watoto watatu, akiwemo Kulture mwenye umri wa miaka 6 na Wave mwenye miaka 3, huku mtoto wao wa tatu bado akiwa mchanga jina lake likiwa bado halijatambulishwa.


Licha ya mgogoro unaoendelea, wanandoa hao wameonekana pamoja mara kadhaa, jambo linalozua maswali kuhusu mustakabali wa uhusiano wao. Wakati Cardi B akiendelea na maisha yake bila Offset, mashabiki wake wanatarajia kusikia zaidi kutoka kwake, hasa kuhusu albamu yake mpya inayotarajiwa kuachiwa mwaka huu.

---

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad