P DIDY ACHUNGWA ASIJIUE GEREZANI BAADA YA KUKOSA DHAMANA...



Sean “Diddy” Combs, mwanzilishi wa Bad Boy Records, ameripotiwa kuwekwa chini ya uangalizi maalum ili kuzuia kujiua baada ya kukosa dhamana kufuatia kukamatwa kwake kwa tuhuma za usafirishaji wa binadamu na utapeli wa fedha.

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyozungumza na People, hatua hiyo imechukuliwa kwa ajili ya "tahadhari kwani hali yake ya kiakili haiko sawa." Hivi sasa, Diddy mwenye umri wa miaka 54 anashikiliwa katika gereza la Metropolitan Detention Center (MDC) huko Brooklyn, New York.

MDC lina sifa mbaya ya mazingira machafu, ukatili wa wafungwa, na kuongezeka kwa kesi za kujiua. Mwezi Julai, mfungwa mmoja alifariki baada ya ugomvi ndani ya gereza hilo.

Diddy alifikishwa kwenye mahakama ya Manhattan siku ya Jumanne kwa tuhuma za kuunda mtandao wa uhalifu uliokuwa ukijihusisha na biashara ya ngono, ajira za kulazimishwa, utekaji nyara, na kupindisha haki.Hata hivyo, amekuwa akikana tuhuma hizi huku akiendelea kukabiliwa na mashtaka mengine ya unyanyasaji wa kijinsia

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad