Mwimbaji wa Kundi la P Square lenye maskani yake poa Nchini Nigeria ‘Paul Okoye’ a.k.a 'Rude Boy', amethibitisha rasmi mwisho wa kundi hilo kwa mara nyingine nakuahidi kuwa hatojishughulisha na mchongo wowote kuhusu kundi hilo.
Katika taarifa yake ya hivi majuzi, amelezea kusikitishwa kwake na mienendo ya kundi hilo, akiangazia kuwa aliwajibika kwa kazi nyingi huku wengine wakinufaika sawa.
“Nimepambana sana kuijenga P-Square, mithili ya mkulima ambae amestawisha mahindi yake vema nakungoja mavuno, lakini nyani wanavamia nakuyala yote nakumsababishia hasara, Sifanyi tena!!” amefunguka ‘Rude Boy’ baada takuulizwa na mashabiki ambao wanahitaji muunganiko wake na pacha wake ‘Peter Okoye’ a.k.a ‘Mr P’.
Baadhi ya Wanigeria wamemkosoa ‘Rude Boy’, juu ya uamuzi huo badala yakutafuta suluhu kwa maslahi ya mashabiki wao. Hata hivyo pacha wake, ‘Mr P’ ameendelea kusisitiza kuwa kuanguka kwao kumesababishwa na Kaka yao mkubwa ‘Jude Okoye’ ambae ndie meneja wa kundi hilo, kuwa kikwazo kikubwa kwenye biashara kutokana na kujinufaisha zaidi.