Producer Bob Manecky Amvulia Kofia Producer S2Kizzy

Producer Bob Manecky Amvulia Kofia Producer S2Kizzy


Producer mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Bob Manecky, ameonyesha heshima kubwa kwa kazi ya producer wa kizazi kipya, S2kizzy. Kupitia Instagram, Bob Manecky aliandika "Zombie Kashindikana," ikimaanisha kuwa S2kizzy ameonyesha umahiri mkubwa katika utayarishaji wa muziki, ambao kwa sasa unashikilia chati nyingi za hits kwenye soko la muziki wa Bongo Fleva.


Maneno haya kutoka kwa Bob Manecky, ambaye ni mmoja wa watu wa heshima katika sekta ya muziki nchini, ni ishara ya kuthibitisha ubora wa kazi za @s2kizzy,. Akishea ujumbe huo kwenye akaunti yake, S2kizzy alionekana kufurahia sana kupongezwa na mmoja wa waliomtangulia katika tasnia.


S2kizzy kwa sasa amekuwa producer anayehusishwa na mafanikio ya nyimbo nyingi zinazotikisa nchini na kimataifa, akiendelea kuleta ladha mpya na mitindo tofauti katika muziki wa Bongo Fleva. Pongezi kama hizi kutoka kwa mastaa wakongwe kama @bobmanecky zinaonyesha jinsi ambavyo kizazi kipya kinaendelea kusukuma mbele muziki wa Tanzania na kufungua milango mipya kimataifa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad