RAIS SAMIA: KUITA SERIKALI YA WAUAJI SIO SAWA

RAIS SAMIA: KUITA SERIKALI YA WAUAJI SIO SAWA

“Siku kadha zilizopita Ndugu zangu Nchi yetu imepata msiba wa kuuawa kwa mmoja wa Kiongozi wa CHADEMA, kifo kilichosisimua miili na akili za Watanzania na kuibua hisia kali hasa kwa Wafuasi wa Chama hicho, katika hali ya kushangaza kifo hicho kimeleta hisia kali pia kwa Wawakilishi wa baadhi ya Mataifa ya Nje wanaowakilisha Nchi zao hapa kwetu, nataka niungane nao na niseme kwamba kwasababu yoyote ile mauaji haya hayakubaliki na ndio maana Serikali tuliyalaani na kutaka uchunguzi wa haraka ufanyikke na ndivyo inavyofanyika Duniani kote”


“Nadhani nyie ni Mashahidi kule kwa wenzetu kulikoendelea kuna Mwanasiasa amekoswa kuuawa mara mbili (Trump) lakini tulichokisikia ni Serikali kutaka uchunguzi ufanyike kwahiyo si ajabu na kwetu baada ya tukio kutaka uchunguzi ufanyike na kazi nimeambiwa inaendelea vizuri”


“Baada ya tukio la Mzee Kibao nimekuwa nikiangalia maoni ya Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Viongozi wa Dini baadhi yao wakiniomba nikemee mambo hayo, maoni ya Wazee mashuhuri nimemsikia Mzee wetu Butiku nae kasema, Wawakilishi wa Mataifa ya Nje hapa Nchini nao wametoa tamko, Jumuiya za Kiraia na Wananchi kwa ujumla na wenyewe wamesema waliyosema “


“Hisia za makundi yote niliyotaja zikiibuliwa na kifo kimoja tu cha Ndugu yetu Kibao lakini kuna vifo vinasemwa muda baada ya muda, Watoto Albino wanauliwa, Watoto wadogo wanauliwa, sijui Mzee kahisiwa uchawi kauliwa mpaka leo Watoto watatu wamekutwa wameuliwa huko Dodoma”


“Inashangaza kifo cha Ndugu yetu kibao kimeibua wimbi kubwa, kulaani, kusikitika, kulaumu kuita Serikali ya wauaji, kufanyaje, hii sio sawa, kifo ni kifo, tunachotakiwa kufanya Watanzania wote tukemeeane, tusimame imara kukemea mambo haya, damu ya Mtanzania ituume tusiwe tunamwaga damu bila sababu” —— Rais wa Tanzania, Dkt. Samia kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro leo September 17,2024

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad