RAIS SAMIA: WAMEPANGA SAMIA AONDOKE, HAIENDI HIVYO

 “Nilikuwa nasikiliza kwa makini maelezo yaliyotolewa na Katibu Mkuu CCM, nimerushiwa na nimeisikiliza vizuri sana clip ya Mh. Slaa wa CHADEMA na clip ya Joseph Yona wa Chalinze wote wakitoa taswira ya mipango ya uvunjifu wa amani inayopangwa na baadhi ya Vyama vya Siasa”


“Nayaunganisha haya na maamuzi ya kikao cha September 11,2024 kilichofanywa na Chama kimoja cha siasa kule Ngurero Mkoani Arusha kikao ambacho kimeazimia kuwatumia na kuwachochea Vijana kwa kuzusha tuhuma dhidi ya Jeshi la Polisi, kufanya siasa chonganishi kwenye misiba na kushusha morali kwa Jeshi la Polisi ya kufanya kazi yao ya kulinda usalama wa Raia na mali zao”



RAIS SAMIA: WAMEPANGA SAMIA AONDOKE, HAIENDI HIVYO


“Nashukuru katika kikao hichohicho mkutano ulibaini na ulitambua kwamba Nchi hii ya Tanzania ina intelejensia kubwa na kwamba walipeana onyo wanapofanya mipango ya miovu watumie vema fursa waliyoipata kwenye R4 ili mipango ile waseme si tumeruhusiwa, falsafa ya R4 imeturuhusu, kwahiyo wanafanya mipango yao miovu huko”


“Nashukuru kwamba wametambua kwamba Nchi hii ina intelejensia kubwa na ushahidi ni kwamba yote yaliyosemwa kule mie ninayo, huo ndio ubora wa intelejensia yetu, nataka niwaambie, vikao vyote vitakavyopanga uovu, uovu unaopangwa tutaupata, kumepangwa sijui kushushwa moto mpaka Samia aseme ‘basi nime-surrender naondoka’ hiyo ni Serikali au Serikali ya samaki?, hiyo ni Serikali ya samaki Ndugu zangu maana samaki kila akiwa mkubwa na akili inapungua”


“Hiyo ni Serikali ya samaki lakini Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haiondoshwi hivyo, sasa kwa kutumia kofia ya Amiri Jeshi Mkuu katika Nchi hii niseme kwamba tumeapa kuilinda na kuitetea katiba ya Tanzania na tutafanya kila linalowezekana kuimairisha ulinzi na usalama wa Tanzania kwakuwa ni jukumu letu, kwenye wajibu huu wala hatuitaji kuelekezwa na yoyote nini cha kufanya “—— Rais wa Tanzania, Dkt. Samia kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro leo September 17,2024

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad