Alipigwa kisu wakati akihudhuria mazishi ya kiongozi wa kidini karibu na mji mkuu Moroni lakini alijeruhiwa "kidogo tu" na amerejea nyumbani tangu wakati huo, msemaji Fatima Ahamada aliiambia shirika la habari la Reuters.
Aliongeza kwamba mshambuliaji amekamatwa na dhumuni la shambulio hilo bado halijaeleweka.
Utambulisho wa mshambuliaji haujawekwa hadharani lakini ripoti kadhaa zinaashiria kwamba ni afisa kijeshi mchanga.
Mashahidi waliliambia shirika la habari la AFP kwamba walimuona mwanaume huyo ndani ya chumba, akiwa amevaa vazi, ambapo waombolezaji walikuwa wanatoa heshima kwa marehemu.
Wanasema mshambuliaji alijeruhi mkono wa rais wakati wa shambulio hilo, kabla ya kusimamishwa na mmoja wa waombolezaji.