ROMA AMCHANA WAKAZI KUBISHANA NA WANAWAKE....



Majibizano mapya yameibuka, ambapo Roma Mkatoliki amemkosoa rapa Wakazi kwa kupenda kubishana na wanawake. Kupitia akaunti yake ya X (zamani Twitter), Roma aliandika akimchana Wakazi kwa kusema, "Sema mwanetu anapaisha sana Gozi!! Unaanzaje kubishana na mabinti!! Juzi Rosa Ree, Leo Diva!! Ndio kahamia huko?"

@Wakazi hakukaa kimya na alimjibu Roma akimkumbusha kuhusu changamoto zake za zamani, ikiwemo kukosa hela ya chakula na kuomba msaada kwa Shilole, huku akimdhihaki kwa kutoonyesha uadilifu wa kumhoji. Wakazi aliongeza kuwa yeye hulipia chakula kwa Shishi Food na kwamba hajibishani na wanawake bali huwakanya.

@Roma_zimbabwe, kwa upande wake, aliendelea kumjibu, akimwambia Wakazi kuwa ni fursa kujifunza kutokana na changamoto, huku akisisitiza kuwa wengine walitumia matatizo yao kutengeneza muziki na kupata faida. Ugomvi huu umepokelewa na mashabiki kwa mitazamo tofauti, huku ukionekana kuongeza msisimko kwenye anga la burudani. Upi ni upande wako?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad