Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa Cameroon Samuel Etoo ametajwa kuwa miongoni mwa watu wanaowania kiti cha Urais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Etoo ambaye sasa ni Rais wa Chama cha Soka Cameroon (FECAFOOT) anajiandaa kuwania kiti hicho ambacho kipo chini ya Patrice Motsepe.
Taarifa kutoka CAF ambayo makao yake makuu yako nchini Misri inasema kuwa Eto’o anajiandaa kukiwania kiti hicho katika uchaguzi ujao.
Kwa mujibu wa ripoti nyingi, muhula wa Rais wa sasa, Motsepe, unatarajiwa kumalizika mwakani, huku Motsepe akiwa bado hajazungumza kuhusu kugombea tena.
Taarifa kutoka Cameroon zinasema Eto’o anamtaarisha mshauri wake Mongue Nyamsi, kumrithi kama bosi wa FA wa Cameroon atakapoondoka.