UWEPO wa washambuliaji zaidi ya wawili katika Klabu ya Yanga unatoa picha kwamba kazi ipo katika eneo hilo kwa kuwa hakuna mwenye uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza kwenye mechi za ushindani kitaifa na kimataifa msimu wa 2024/25.
Ukiweka kando washambuliaji ndani ya Yanga kuna viungo zaidi ya wawili wenye uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi za mabao na ilikuwa hivyo msimu wa 2023/24 ambapo Aziz Ki yeye ni kiungo mshambuliaji aliibuka kuwa mfungaji bora ndani ya ligi alipofunga jumla ya mabao 21 uwanjani.
Katika eneo la ushambuliaji Yanga ni Prince Dube huyu amekuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambapo amekuwa akiwaweka benchi Clement Mzize.
Kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar Dube alifanya majaribio zaidi ya manne licha ya kukwama kufunga kwenye mchezo huo na hakukomba dakika 90 kweye mchezo huo huku mshambuliaji mwingine Clement Mzize yeye alifunga bao katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar akitokea benchi ilikuwa Agosti 29 2024.
Mshambuliaji mwingine ni Kennedy Musonda na Jean Baleke hawa wote ni washambuliaji ndani ya Yanga. Baleke ni ngizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga na aliwahi kucheza kikosi cha Simba msimu wa 2023/24 alipofunga mabao 8 ndani ya ligi kabla ya kukutana na Thank You.
Gamondi amesema kuwa kila mchezaji ana nafasi ya kucheza ndani ya kikosi hicho malengo ikiwa ni kupata matokeo mazuri kwenye mechi ambazo wanacheza uwanjani.
“Kila mchezaji ana nafasi ya kucheza ndani ya Yanga kwa kuwa wachezaji wote wana uwezo mkubwa na ninafurahishwa na namna ambavyo wanafanya kikubwa ni kuona kwamba kila mchezaji anatimiza majukumu yake.”