Katika episode yake mpya ya podcast yake "Collect Call With Suge Knight", Suge Knight ametoa onyo kwa Sean “Diddy” Combs kuhusu kesi inayomkabili ya usafirishaji haramu wa binadamu na njama za kihalifu zinazohusishwa na kampuni ya Combs Enterprise. Suge, ambaye kwa sasa yuko gerezani, alitumia muda huo kumuelezea Diddy kwamba anafahamu “siri” nyingi zinazohusiana na yanayompata staa huyo.
Kwenye mazungumzo hayo, Suge Knight alieleza kuwa maisha ya Diddy yako hatarini kwa sababu ya siri hizo, akiongeza kuwa kuna watu wenye nia ya kumdhuru. “Puffy, maisha yako yako hatarini kwa sababu unajua siri za nani anayehusika na kile chumba kidogo cha siri mnachoshiriki mambo yenu” alisema Suge. “Unajua watajaribu kukumaliza kama wataweza".
Suge Knight pia alimpa Diddy ushauri kuhusu hali anayoweza kukutana nayo akiwa gerezani. Aliendelea kusema, “Nitakupa ushauri wa kweli, mambo mawili ya haraka. Lazima ufanye uamuzi. Ukifika gerezani, ama utakuwa ukikojoa umesimama au umekaa chini. Nakushauri ujaribu njia ya kwanza, maana ukikaa ndio ukojoe, unajua inamaanisha nini.”
Kwa mujibu wa Knight, jina la "Brother Love" ambalo Diddy amekuwa akilitumia kwa muda, haliwezi kumsaidia akiwa gerezani. Alisema, “Usitumie jina Brother Love ukiwa gerezani, hilo sio jina zuri huko ndani.”
Kesi inayomkabili Diddy imeibua wasiwasi mkubwa kwenye ufalme wake wa biashara, na ikiwa atapatikana na hatia, anatarajiwa kukumbana na adhabu kali. Kesi ya RICO inayomkabili inaweza kumfunga maisha gerezani, huku kesi ya usafirishaji haramu wa binadamu ikiwa na adhabu usiyopungua miaka 15 na au kifungo cha maisha.
Madai hayo ya kusafirisha watu kwa nia ya kuwafanyisha ukahaba pia yanaweza kumletea adhabu ya miaka 10 gerezani. Hali hii imeweka giza kwenye mafanikio makubwa ya biashara na muziki wa Diddy, huku ulimwengu ukiangalia kwa karibu mwenendo wa kesi hiyo.
Pakua Mtandao Mpya wa Kijamii wa Onasasa kupitia Google Play kufuatilia habari zetu zingine. Pia Ona Sasa ni fursa kwa Content Creators kujipatia kipato.