TLS Wafunguka Mauji ya Mzee Kibao

TLS Wafunguka Mauji ya Mzee Kibao


Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimekemea ukosefu wa taarifa kutoka kwa Jeshi la Polisi kuhusu watu waliotekwa kinyume na sheria.

Katika tamko lao la tarehe 10 Septemba 2024 lililotolewa na Baraza la Uongozi la TLS chini ya Rais wake Boniface Mwabukusi, kumetolewa wito kwa Jeshi la Polisi kutoa maelezo ya wazi kuhusu hatua walizochukua katika kushughulikia matukio haya.

Katika tamko lao, TLS imeomba kuvunjwa kwa vikosi kazi ambavyo vimekuwa vikidaiwa kufanya kazi nje ya sheria, na kuhakikisha kuwa ukamataji wowote unafuata taratibu za kisheria.

"Jeshi la Polisi lihakikishe kwamba linatoa taarifa sahihi kwa umma dhidi ya watu wote waliochukuliwa na kutekwa kinyume na sheria," TLS ilisisitiza.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad