Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwezekano wa kutokea kwa upepo mkali unaozidi Kilomita 40 kwa saa, kwa siku tatu mfululizo kuanzia Septemba 1 hadi Septemba 3, 202
Taarifa hiyo imewataka watu kuchukua tahadhari ikisema Athari zinazoweza kujitokeza ni kuathirika na kughairishwa kwa baadhi ya shughuli za Baharini na kuharibika kwa miundombinu ya bahari
Baadhi ya maeneo yatakayoathiriwa ni Ukanda wa Pwani ya Kusini mwa Bahari ya Hindi katika Mikoa ya #Lindi na #Mtwara, baadhi ya maeneo ya Kusini mwa Ziwa Tanganyika, Mikoa ya Rukwa na Katavi, maeneo ya ukanda wa Pwani ya Kaskazini mwa Bahari ya Hindi katika Mikoa ya Dar, Tanga, Pwani, Visiwa vya Mafia na Visiwa vya Unguja na Pemba