Treni ya Mwendokasi inayofanya safari zake Dar es salaam - Dodoma, ilisimama kwa saa kadhaa maeneo ya Ngerengere usiku wa kuamkia leo September 10,2024 na baadhi abiria wakajirekodi video wakionesha kuwa wamesimama katika eneo hilo.
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeomba radhi kwa abiria kutokana na kuchelewa kwa safari kulikosababishwa na changamoto zilizo nje ya uwezo wao ambapo wamesema sababu ya kusimama huko ni pamoja na kusubiri kupishana na treni iliyokuwa ikitoka Dar es salaam kuelekea Morogoro.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano-TRC, Jamila Mbarouk ameiambia @AyoTV_ kuwa “Baadae changamoto zilitatuliwa na huduma za usafirishaji ziliendelea kutolewa, TRC inaomba radhi kwa changamoto zinazojitokeza na inaahidi kuendelea kuzifanyia kazi”