HAKI ZA BINADAMU: Uongozi wa Kampuni ya Mabasi ya Tashriff umesema tukio la kutekwa kwa aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA, Ali Kibao ndani ya basi lao liliwashtua na walishindwa kuzuia kutokana na wahusika kuwa na silaha za moto na waliwatisha wafanyakazi waliokuwa ndani ya basi hilo
Kwa mujibu wa tovuti ya #Mwananchi, Msimamizi wa Mabasi hayo, Shabani Mbeta amesema “Mzee Kibao namfahamu ni mteja wetu wa muda mrefu, tulishangazwa na tukio hilo na limetuliza. Watu walikuwa na silaha za moto na walitutisha kwenye gari letu ambalo walilizuia kwa mbele na nyuma"
Aidha Uongozi wa Kampuni ya Mabasi ya Tashriff umesema mtu aliyekuwa ndani ya basi hilo na kuambatana na watekaji alikataa kutoa taarifa zake mwanzo wa safari lakini baada ya kulazimishwa alizitoa kasoro namba yake ya simu na taarifa zake za tiketi zimeshawasilishwa kwa Polisi