VITA YA SIMBA NA YANGA IMEANZA UPYAA PATACHIMBIKA

 

VITA YA SIMBA NA YANGA IMEANZA UPYAA PATACHIMBIKA



LIGI Kuu Bara inazidi kuchangamka ambapo kwa muda mrefu pale kileleni hujaiona Simba, Azam wala Yanga ikikaa. Fountain Gate na Singida Black Stars zimekuwa zikipishana.

Kidogo afadhali kwa Mnyama Simba imewahi kukaa pale juu msimu huu baada ya kushinda mechi mbili za kwanza kabla ya kuanza majukumu ya michuano ya kimataifa ikishiriki Kombe la Shirikisho Afrika, lakini Yanga na Azam bado hazijaonja baridi la kileleni.

Wababe hao wamekuwa washindani wakubwa tangu mwaka 2008 wakati ambao Azam ilianza kushiriki Ligi Kuu Bara. Ushindani wao unakufanya ufikirie jambo moja kubwa kwamba linapokuja suala la kuwania ubingwa, lazima uwatazame wao.

Rekodi zinaonyesha kwamba tangu mwaka 2008 wakati Azam ikianza kushiriki Ligi Kuu Bara, ni takribani misimu 16 sasa ambapo timu hizo tatu pekee ndizo zimefanikiwa kubeba ubingwa.

Azam ikichukua mara moja msimu wa 2013-2014, wakati Yanga ikibeba mara 9 na Simba 6. Kabla ya hapo, kuanzia mwaka 2001, Simba na Yanga pekee ndiyo zilikuwa zikibadilishana kombe hilo.

Hiyo inatosha kusema moja kwa moja kwamba watatu hao ndiyo washindani wakubwa wa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ingawa mbele ya safari lolote linaweza kutokea kwa timu nyingine kuingilia vita hiyo.

Kilichotokea msimu uliopita ambapo Yanga ilijihakikishia ubingwa wa ligi zikisalia mechi tatu, huku vita ya Azam na Simba kuwania nafasi ya pili ikiamuliwa katika mechi za kufungia msimu, ndicho kinatarajiwa kutokea msimu huu.

Hiyo inatokana na namna ambavyo timu hizo zilivyoanza msimu huu ambapo jana Jumapili zote zilikuwa uwanjani kila moja ikipambania pointi tatu. Yanga ikiwa nyumbani dhidi ya KMC, Simba ugenini kwa Dodoma Jiji na Azam ugenini kwa Mashujaa.

Kabla ya mechi hizo za jana, msimamo wa ligi ulikuwa ukionyesha Fountain Gate ipo kileleni na pointi zake 13 baada ya kushuka dimbani mara sita, ikifuatiwa na Singida Black Stars yenye 12 na mechi zake tano.

Simba ilikuwa nafasi ya tatu ikiwa na pointi tisa zilizotokana na kushinda mechi zote tatu za kwanza kabla ya jana, huku Azam iliyofungwa na Simba 2-0, ilikuwa nafasi ya nne ikikusanya pointi nane katika mechi tano. Yanga ndiyo timu iliyokuwa na mechi chache zaidi ambazo ni mbili ikiwa imeshinda zote na kupata pointi sita.

HALI ILIVYO

Vita ya wababe hao watatu, Azam, Simba na Yanga inatarajiwa kuendeleza tena msimu huu ukizingatia kwamba Azam wana rekodi yao ambayo wamekuwa wakiifukuzia kwa misimu mitatu mfululizo sasa.

Timu hiyo ikiwa chini ya kocha mpya raia wa Morocco, Rachid Taoussi, ina kazi kubwa ya kuzipiku pointi za msimu uliopita ambazo ni 69.

Simba na Yanga nao wana vita yao ya watani wa jadi, kila mmoja akipambana kuchukua ubingwa wa Ligi kuu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad