WASHTAKIWA WALIOTUMWA NA AFANDE WAKUTWA NA KESI YA KUJIBU

 

WASHTAKIWA WALIOTUMWA NA AFANDE WAKUTWA NA KESI YA KUJIBU

Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imewakuta na kesi ya kujibu washitakiwa wote wanne wa kesi ya kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume na maumbile binti ambaye ni mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam.


Washitakiwa hao wamekutwa na kesi ya kujibu leo Jumatatu, Septemba 23, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Zabibu Mpangule hivyo watatakiwa kujitetea kuanzia Jumatano ya Septemba 25 na 26, 2024.


Washitakiwa hao wamekutwa na kesi ya kujibu baada ya upande wa Jamhuri kuleta jumla ya vielelezo 12 na mashahidi 18 ambao walitoa ushahidi kuhusu kesi inayowakabili washitakiwa wanne ambao ni Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), MT 140105 Clinton Damas, maarufu Nyundo, Askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.


Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama leo Jumatatu, wakili wa washitakiwa hao, Godfrey Wasonga amesema Mahakama imetoa uamuzi kuwa washitakiwa wote wana kesi ya kujibu na wanatakiwa kujitetea Septemba 25 na 26, 2024 na wao wameshajipanga.


Wasonga amesema washitakiwa wote wanne watajitetea kwa kula kiapo ambapo kutakuwa na mashahidi 10 na vielelezo sita ambavyo vitatumika kwenye ushahidi wao.


Washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Agosti 19, 2024 ambapo walisomewa mashitaka mawili ya kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume na maumbile binti mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar sa Saalam ambapo walikana mashitaka yanayowakabili.


Kutokana na unyeti wa kesi hiyo upande wa mwendesha mashtaka wa Serikali ulipanga kusikiliza kesi hiyo mfululizo ambapo washitakiwa waliendelea kusota rumande kuanzia Agosti 20 hadi sasa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad