AFANDE ALIYETAJWA KWENYE KESI YA BINTI WA YOMBO, SIO MWANAMKE


AFANDE ALIYETAJWA KWENYE KESI YA BINTI WA YOMBO, SIO MWANAMKE

Kwanini huyu Afande anayehusika kwanini hajashtakiwa? Tumefanya vikao sana na mwendesha mashtaka Dodoma yaani mpaka kesi inakamilika sisi tulipiga kambi Dodoma Mimi na mwenzangu wa Mkuki. Katika majadiliano ili mtuhumiwa yoyote apelekwe mahakamani sheria ilivyo sasa hivi ni lazima ufanyike uchunguzi na ushahidi wa kutosheleza kumpeleka mtuhumiwa mahakamani. Sasa connection ya huyu mama, huyu Afande anayetajwa ingetokea wakati gani?

"Wakati uchunguzi unaendelea wakati wanawahoji wale washtakiwa pamoja na binti mwenyewe hakuna yoyote kati ya wale aliyemwingiza yule Afande tunayemsikia yule Afande Fatma Kigondo. Hakuna aliyemuingiza kwenye ule mchezo.

"Binti alivyohojiwa alisema alikuwa akionyeshwa picha anasema aliambiwa aombe radhi kwa Afande lakini picha aliyokuwa akionyeshwa ni picha ya mwanaume aliyevaa magwanda ya kijeshi"- Wakili Edwin Mugambila ¢¢- Mtendaji Mkuu wa Mtandao Wa Kitaifa Wa kupinga usafirishaji haramu Wa Binadamu akieleza akipitia 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad